Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 41 - يُوسُف - Page - Juz 12
﴿يَٰصَٰحِبَيِ ٱلسِّجۡنِ أَمَّآ أَحَدُكُمَا فَيَسۡقِي رَبَّهُۥ خَمۡرٗاۖ وَأَمَّا ٱلۡأٓخَرُ فَيُصۡلَبُ فَتَأۡكُلُ ٱلطَّيۡرُ مِن رَّأۡسِهِۦۚ قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ ٱلَّذِي فِيهِ تَسۡتَفۡتِيَانِ ﴾
[يُوسُف: 41]
﴿ياصاحبي السجن أما أحدكما فيسقي ربه خمرا وأما الآخر فيصلب فتأكل الطير﴾ [يُوسُف: 41]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Enyi marafiki wangu gerezani, haya uchukueni uaguzi wa ndoto zenu: ama yule aliyeona kwenye ndoto yake kuwa anakamua zabibu, yeye atatoka jela na atakuwa ni mwenye kuishughulikia pombe ya mfalme. Ama mwingine aliyeota kuwa anabeba mkate juu ya kichwa chake, yeye atasulubiwa na aachwe, na ndege waje wamle kichwa chake. Limeshapitishwa jambo ambalo mlikuwa mnaliuliza na limeshamalizwa.» |