Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 16 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿قُلۡ مَن رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ قُلِ ٱللَّهُۚ قُلۡ أَفَٱتَّخَذۡتُم مِّن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَ لَا يَمۡلِكُونَ لِأَنفُسِهِمۡ نَفۡعٗا وَلَا ضَرّٗاۚ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُ أَمۡ هَلۡ تَسۡتَوِي ٱلظُّلُمَٰتُ وَٱلنُّورُۗ أَمۡ جَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ خَلَقُواْ كَخَلۡقِهِۦ فَتَشَٰبَهَ ٱلۡخَلۡقُ عَلَيۡهِمۡۚ قُلِ ٱللَّهُ خَٰلِقُ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُوَ ٱلۡوَٰحِدُ ٱلۡقَهَّٰرُ ﴾
[الرَّعد: 16]
﴿قل من رب السموات والأرض قل الله قل أفاتخذتم من دونه أولياء﴾ [الرَّعد: 16]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Waambie washirikina, ewe Mtume, «Ni nani muumba mbingu na ardhi na mwenye kuziendesha?» Sema, «Mwenyezi Mungu Ndiye Muuumba Mwenye kuziendesha. Na nyinyi mnalikubali hilo.» Kisha waambie ukiwalazimisha hoja, «Je, mnawafanya wasiokuwa Yeye ni waabudiwa wenu, na hali ya kuwa wao hawawezi kuzinufaisha nafsi zao au kuzidhuru, wacha kule kuwanufaisha nyinyi au kuwadhuru, na mkaacha kumuabudu mwenye kuwamiliki wao?» Waambie, «Kwani analingana kwenu nyinyi kafiri, ambaye ni kama kipofu, na Muumini, ambaye ni kama anayeona? Au kwani unalingana kwenu nyinyi ukafiri, ambao ni kama giza, na Imani, ambayo ni kama mwangaza? Au ni kwamba wale wasimamizi wao wanaowafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu wanaumba kama Anavyoumba, vikawatatiza viumbe vya washirika na viumbe vya Mwenyezi Mungu, ndipo wakaitakidi kwamba wao wanastahiki kuabudiwa?» Waambie, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu Aliyetukuka ni Muumba kila kilichoko ambacho hakikuwako; Yeye Ndiye Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake na Yeye Ndiye Aliye mmoja Mwenye kutendesha nguvu Anayestahiki uungu na ibada, na sio masanamu na mizimu isiyodhuru wala kunufaisha.» |