Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 17 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَسَالَتۡ أَوۡدِيَةُۢ بِقَدَرِهَا فَٱحۡتَمَلَ ٱلسَّيۡلُ زَبَدٗا رَّابِيٗاۖ وَمِمَّا يُوقِدُونَ عَلَيۡهِ فِي ٱلنَّارِ ٱبۡتِغَآءَ حِلۡيَةٍ أَوۡ مَتَٰعٖ زَبَدٞ مِّثۡلُهُۥۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡحَقَّ وَٱلۡبَٰطِلَۚ فَأَمَّا ٱلزَّبَدُ فَيَذۡهَبُ جُفَآءٗۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ فَيَمۡكُثُ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡأَمۡثَالَ ﴾
[الرَّعد: 17]
﴿أنـزل من السماء ماء فسالت أودية بقدرها فاحتمل السيل زبدا رابيا ومما﴾ [الرَّعد: 17]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kisha Mwenyezi Mungu Akapiga mfano wa ukweli na urongo kuwa ni kama maji Aliyoyateremsha kutoka juu, yakapita kwenye mabonde ya ardhi kwa kadiri ya udogo wake na ukubwa wake, mikondo ya maji ikabeba povu likiwa juu yake lisilo na faida. Na akapiga mfano mwingine wa madini ambayo watu huyachoma moto ili kuyayeyusha kutaka kutengeneza pambo, kama vile dhahabu na fedha, au kutaka manufaa ya kujinufaisha, kama vile shaba, ukatoka uchafu wake usio na faida kama ule uliokuwa pamoja na maji. Kwa mfano huu, Mwenyezi Mungu Apigia mfano ukweli na urongo. Urongo ni kama povu la maji, linapotea au linatupwa kwa kuwa halina faida, na ukweli ni kama maji safi na madini yaliyotakasika, yanasalia kwenye ardhi kwa kunufaika nayo. Kama Alivyowafafanulia nyinyi mifano hii, hivyo ndivyo Anavyoipiga kwa watu upate kufunuka wazi ukweli ujitenge na urongo, na uongofu ujitenge na upotevu |