×

Na kama ingeli kuwako Qur'ani ndiyo inayo endeshewa milima, na kupasuliwa ardhi, 13:31 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Ar-Ra‘d ⮕ (13:31) ayat 31 in Swahili

13:31 Surah Ar-Ra‘d ayat 31 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 31 - الرَّعد - Page - Juz 13

﴿وَلَوۡ أَنَّ قُرۡءَانٗا سُيِّرَتۡ بِهِ ٱلۡجِبَالُ أَوۡ قُطِّعَتۡ بِهِ ٱلۡأَرۡضُ أَوۡ كُلِّمَ بِهِ ٱلۡمَوۡتَىٰۗ بَل لِّلَّهِ ٱلۡأَمۡرُ جَمِيعًاۗ أَفَلَمۡ يَاْيۡـَٔسِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن لَّوۡ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَهَدَى ٱلنَّاسَ جَمِيعٗاۗ وَلَا يَزَالُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ تُصِيبُهُم بِمَا صَنَعُواْ قَارِعَةٌ أَوۡ تَحُلُّ قَرِيبٗا مِّن دَارِهِمۡ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ وَعۡدُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ ﴾
[الرَّعد: 31]

Na kama ingeli kuwako Qur'ani ndiyo inayo endeshewa milima, na kupasuliwa ardhi, na kusemeshewa wafu, (basi ingeli kuwa Qur'ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua walio amini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu ange penda bila ya shaka angeli waongoa watu wote? Wala walio kufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa waliyo yatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ولو أن قرآنا سيرت به الجبال أو قطعت به الأرض أو كلم, باللغة السواحيلية

﴿ولو أن قرآنا سيرت به الجبال أو قطعت به الأرض أو كلم﴾ [الرَّعد: 31]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anawarudi makafiri ambao walitaka kwamba Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ateremshiwe miujiza yenye kuonekana, kwakuwaambia, «Lau kulikuwa na Qur’ani itakayosomwa ikafanya majabali yaondoke mahali pake au ardhi ipasuke itoe mito au wafu wafufuke na waseme, kama walivyotaka kwako, hii Qur’ani ingalikuwa ndiyo yenye kusifika na hayo na si kitu kingine, na pia hawangaliamini.. Bali ni ya Mwenyezi Mungu amri juu ya miujiza na mengineyo. Kwani hawakujua Waumini kwamba lau Mwenyezi Mungu Anataka, watu wote wa ardhini wangaliamini bila ya miujiza? Na hawataacha makafiri kuendelea kuteremkiwa na mkasa kwa sababu ya ukafiri wao, kama kuuawa na kutekwa katika vita vya Waislamu, au kuteremkiwa na mkasa huo karibu na nyumba zao, mpaka ahadi ya Mwenyezi Mungu ije ya kuwapa ushindi juu yao. Hakika Mwenyezi Mungu Haendi kinyume na ahadi Yake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek