Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 30 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿كَذَٰلِكَ أَرۡسَلۡنَٰكَ فِيٓ أُمَّةٖ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهَآ أُمَمٞ لِّتَتۡلُوَاْ عَلَيۡهِمُ ٱلَّذِيٓ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ وَهُمۡ يَكۡفُرُونَ بِٱلرَّحۡمَٰنِۚ قُلۡ هُوَ رَبِّي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ مَتَابِ ﴾
[الرَّعد: 30]
﴿كذلك أرسلناك في أمة قد خلت من قبلها أمم لتتلو عليهم الذي﴾ [الرَّعد: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kama tulivyowatuma Mitume kabla yako, tulikutuma, ewe Mtume, katika ummah waliopita kabla yao ummah wa Mitume, ili uwasomee ummah huu Qur’ani iliyoteremshwa kwako, na hali ya watu wako ni kuukanusha upweke wa Mwingi wa rehema. Waambie, ewe Mtume, «Mwingi wa rehema Ambaye hamkumpwekesha na mkamfanya ni Mola mmoja Ndiye Mola wangu, Peke Yake; hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Kwake Yeye nimetegemea na nina imani, na Kwake Yeye ndio marejeo yangu na makimbilio yangu |