Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 38 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا رُسُلٗا مِّن قَبۡلِكَ وَجَعَلۡنَا لَهُمۡ أَزۡوَٰجٗا وَذُرِّيَّةٗۚ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأۡتِيَ بِـَٔايَةٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ لِكُلِّ أَجَلٖ كِتَابٞ ﴾
[الرَّعد: 38]
﴿ولقد أرسلنا رسلا من قبلك وجعلنا لهم أزواجا وذرية وما كان لرسول﴾ [الرَّعد: 38]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka waliposema, «Una nini, ewe Mtume, unaoa wanawake?» Hakika tulituma kabla yako Mitume kati ya wanadamu na kuwafanya wawe na wake na watoto. Na pia utaje waliposema, «Lau alikuwa ni Mtume angalituletea miujiza tuliyoitaka.» Haiko kwenye uwezo wa Mtume yoyote, kuleta miujiza ambayo watu wake waliitaka isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila jambo alilolihukumu Mwenyezi Mungu lina maandishi na wakati, Mwenyezi Mungu Ameliandika hapo Kwake, halitangulii wala halichelewi |