Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 37 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿وَكَذَٰلِكَ أَنزَلۡنَٰهُ حُكۡمًا عَرَبِيّٗاۚ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم بَعۡدَ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا وَاقٖ ﴾
[الرَّعد: 37]
﴿وكذلك أنـزلناه حكما عربيا ولئن اتبعت أهواءهم بعد ما جاءك من العلم﴾ [الرَّعد: 37]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kama tulivyowateremshia Mitume Vitabu kwa lugha zao, tulikuteremshia wewe, ewe Mtume, Qur’ani kwa lugha ya Kiarabu, ili uitumie katika kuhukumu. Na lau ulifuata mapendeleo ya washirikina katika kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, baada ya haki iliyokujia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hutakuwa na msaidizi yoyote mwenye kukuhami na kuzuia adhabu ya Mwenyezi Mungu isikufikie |