Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 42 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿وَقَدۡ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ فَلِلَّهِ ٱلۡمَكۡرُ جَمِيعٗاۖ يَعۡلَمُ مَا تَكۡسِبُ كُلُّ نَفۡسٖۗ وَسَيَعۡلَمُ ٱلۡكُفَّٰرُ لِمَنۡ عُقۡبَى ٱلدَّارِ ﴾
[الرَّعد: 42]
﴿وقد مكر الذين من قبلهم فلله المكر جميعا يعلم ما تكسب كل﴾ [الرَّعد: 42]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika wale waliokuwa kabla yao waliwapangia njama Mitume wao, kama vile hawa walivyokufanyia. Basi vitimbi vyote vina Mwenyezi Mungu, Anatangua vitimbi vyao na kuwarudishia wenyewe wapite patupu na wajute. Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu Kwake, Anakijua kile ambacho kila mtu anakichuma, chema au kibaya, na atalipwa kwa hicho. Na watajuwa makafiri, watakapofika kwa Mola wao, ni nanani atakuwa na mwisho mwema baada ya dunia hii. Huo ni wa wafuasi wa Mitume. Katika haya kuna onyo na tishio kwa makafiri |