Quran with Swahili translation - Surah Ibrahim ayat 9 - إبراهِيم - Page - Juz 13
﴿أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَبَؤُاْ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ قَوۡمِ نُوحٖ وَعَادٖ وَثَمُودَ وَٱلَّذِينَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ لَا يَعۡلَمُهُمۡ إِلَّا ٱللَّهُۚ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَرَدُّوٓاْ أَيۡدِيَهُمۡ فِيٓ أَفۡوَٰهِهِمۡ وَقَالُوٓاْ إِنَّا كَفَرۡنَا بِمَآ أُرۡسِلۡتُم بِهِۦ وَإِنَّا لَفِي شَكّٖ مِّمَّا تَدۡعُونَنَآ إِلَيۡهِ مُرِيبٖ ﴾
[إبراهِيم: 9]
﴿ألم يأتكم نبأ الذين من قبلكم قوم نوح وعاد وثمود والذين من﴾ [إبراهِيم: 9]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani haikuwajia, enyi ummah wa Muhammad, habari za ummah waliowatangulia: watu wa Nūḥ, watu wa Hūd, watu wa Ṣāliḥ na ummah waliokuja baada yao? Hakuna anayeidhibiti idadi yao isipokuwa Mwenyezi Mungu. Mitume wao waliwajia kwa hoja waziwazi, wakaiuma mikono yao kwa hasira na kwa kiburi cha kutoikubali Imani, na wakasema kuwaambia Mitume wao, «Sisi hatuyaamini mliyotuletea, na sisi tuko kwenye shaka yenye kutia wasiwasi juu ya yale unayotuitia kwayo ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kumpwekesha.» |