Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 118 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا مَا قَصَصۡنَا عَلَيۡكَ مِن قَبۡلُۖ وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ ﴾
[النَّحل: 118]
﴿وعلى الذين هادوا حرمنا ما قصصنا عليك من قبل وما ظلمناهم ولكن﴾ [النَّحل: 118]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mayahudi tuliwaharamishia vile vitu tulivyokupa habari zake, ewe Mtume, kabla, navyo ni kila mnyama mwenye kucha na mafuta ya ng’ombe, mbuzi na kondoo, isipokuwa kile kilichobebwa na migongo yao au matumbo yao au kilichotangamana na mifupa. Na sisi hatukuwadhulumu wao , lakini wao walikuwa ni wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa kukanusha na kufanya uadui, ndipo wakastahili kuharamishiwa kwa njia ya kutiwa adabu |