Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 119 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٌ ﴾
[النَّحل: 119]
﴿ثم إن ربك للذين عملوا السوء بجهالة ثم تابوا من بعد ذلك﴾ [النَّحل: 119]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kisha hakika Mola wako, kwa wale waliofanya maasia, kwa kutojua mwisho wake na kwamba yanapasisha hasira za Mwenyezi Mungu - kwani kila anayemuasi Mwenyezi Mungu, kwa kukosea au kwa kusudia, huwa ni mjinga kwa mtazamo huu, hata kama anajua kuwa ni haramu-, kisha wakarudi kwa Mwenyezi Mungu na kuyaepuka yale madhambi waliokuwa wakiyafanya na wakazitengeneza nafsi zao na matendo yao, hakika Mola wako, baada ya kutubia kwao na kutengenea kwao, ni Mwenye kuwasamehe, ni Mwenye huruma kwao |