Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 12 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ وَٱلنُّجُومُ مُسَخَّرَٰتُۢ بِأَمۡرِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ ﴾
[النَّحل: 12]
﴿وسخر لكم اليل والنهار والشمس والقمر والنجوم مسخرات بأمره إن في ذلك﴾ [النَّحل: 12]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Amewadhalilishia usiku kwa mapumziko yenu, na mchana kwa maisha yenu, na Amewadhalilishia jua likawa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na ili mpate kujua miaka na hesabu na manufaa mengine yasiyokuwa hayo. Na nyota huko mbinguni zimedhalilishwa kwa ajili yenu kwa amri ya Mwenyezi Mungu, ili mjue nyakati, kuiva kwa matunda na mazao na pia kuongoka kwa nyota hizo kwenye giza. Hakika, katika kudhalilisha huko, kuna alama waziwazi kwa watu wanaotia mambo akilini mwao kuhusu Mwenyezi Mungu, hoja Zake na alama Zake |