Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 13 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَمَا ذَرَأَ لَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُخۡتَلِفًا أَلۡوَٰنُهُۥٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَذَّكَّرُونَ ﴾
[النَّحل: 13]
﴿وما ذرأ لكم في الأرض مختلفا ألوانه إن في ذلك لآية لقوم﴾ [النَّحل: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Amewadhalilishia vile Alivyowaumbia katika ardhi miongoni mwa vinavyotambaa humo na matunda na madini na visivyokuwa hivyo ambavyo vina rangi na manufaa mbalimbali. Hakika katika uumbaji huo na kutafautiana rangi na manufaa pana mazingatio kwa watu wanaowaidhika na wanaojua kwamba katika kuvidhalilisha vitu hivyi pana alama nyingi juu ya umoja wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na juu ya kumpwekesha kwa ibada |