Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 14 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَهُوَ ٱلَّذِي سَخَّرَ ٱلۡبَحۡرَ لِتَأۡكُلُواْ مِنۡهُ لَحۡمٗا طَرِيّٗا وَتَسۡتَخۡرِجُواْ مِنۡهُ حِلۡيَةٗ تَلۡبَسُونَهَاۖ وَتَرَى ٱلۡفُلۡكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ ﴾
[النَّحل: 14]
﴿وهو الذي سخر البحر لتأكلوا منه لحما طريا وتستخرجوا منه حلية تلبسونها﴾ [النَّحل: 14]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Yeye Ndiye Ambaye Amewadhalilishia bahari ili mpate kula nyama laini ya samaki mnaowavua, na mtoe humo pambo mnalolivaa kama lulu na marjani, na utaziona jahazi kubwa zinapasua uso wa maji zikienda na kurudi, na mnazipanda ili mtafute riziki ya Mwenyezi Mungu kwa kufanya biashara na kutafuta faida ndani yake. Kwani huenda nyinyi mkamshukuru Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa neema zake kubwa juu yenu na msimuabudu asiyekuwa Yeye |