Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 38 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَا يَبۡعَثُ ٱللَّهُ مَن يَمُوتُۚ بَلَىٰ وَعۡدًا عَلَيۡهِ حَقّٗا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[النَّحل: 38]
﴿وأقسموا بالله جهد أيمانهم لا يبعث الله من يموت بلى وعدا عليه﴾ [النَّحل: 38]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hawa washirikina waliapa kwa Mwenyezi Mungu viapo vizito kwamba Mwenyezi Mungu Hatamfufua aliyekufa baada na kumalizika na kutawanyika. Kwani, Atawafufufa Mwenyezi Mungu kwa lazima, hiyo ni ahadi ya kweli Aliyojilazimisha nayo, lakini wengi wa watu hawaujui uweza wa Mwenyezi Mungu wa kufufua, ndio maana wanaukanusha |