Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 59 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿يَتَوَٰرَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ مِن سُوٓءِ مَا بُشِّرَ بِهِۦٓۚ أَيُمۡسِكُهُۥ عَلَىٰ هُونٍ أَمۡ يَدُسُّهُۥ فِي ٱلتُّرَابِۗ أَلَا سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ ﴾
[النَّحل: 59]
﴿يتوارى من القوم من سوء ما بشر به أيمسكه على هون أم﴾ [النَّحل: 59]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Anajificha kwa kuchukia asionekane na watu wake, akiona aibu na kuingiwa na huzuni kwa habari iliyomchukiza ya kuzaliwa mtoto wa kike, huku akiwa ametunduwaa juu ya tukio la mtoto huyo aliyezaliwa: je, amuache kuishi kwenye hali ya unyonge na utwevu au amzike mchangani akiwa hai? Jueni mtanabahi kwamba ni uamuzi mbaya mno wanaouamua ya kuwafanya watoto wa kike ni wa Mwenyezi Mungu na watoto wakiume ni wao |