Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 66 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَإِنَّ لَكُمۡ فِي ٱلۡأَنۡعَٰمِ لَعِبۡرَةٗۖ نُّسۡقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِۦ مِنۢ بَيۡنِ فَرۡثٖ وَدَمٖ لَّبَنًا خَالِصٗا سَآئِغٗا لِّلشَّٰرِبِينَ ﴾
[النَّحل: 66]
﴿وإن لكم في الأنعام لعبرة نسقيكم مما في بطونه من بين فرث﴾ [النَّحل: 66]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa kweli muna nyinyi, enyi watu, mazingatio katika wanyama howa, nao ni ng’ombe, ngamia na mbuzi na kondoo. Kwani mumeshuhudia kwamba sisi tunawanywesha kutoka kwenye nyato zao maziwa yanayotoka kati ya choo, kilicho ndani ya tumbo, na damu yakiwa yamesafishika na kila uchafu, yenye ladha, hayamkeri mwenye kuyanywa |