Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 65 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَٱللَّهُ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَآۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَسۡمَعُونَ ﴾
[النَّحل: 65]
﴿والله أنـزل من السماء ماء فأحيا به الأرض بعد موتها إن في﴾ [النَّحل: 65]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mwenyezi Mungu Ameteremsha mvua kutoka mawinguni, na Akatoa kwa mvua hiyo mimea kutoka ardhini baada ya kuwa kame na kavu. Hakika katika kuteremsha mvua na kuotesha mimea pana ushahidi juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu wa kufufua, na pia pana ushahidi juu ya upweke Wake kwa watu wanaosikia, wanaozingatia, wanaomtii Mwenyezi Mungu na wanaomuogopa |