Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 70 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ ثُمَّ يَتَوَفَّىٰكُمۡۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرۡذَلِ ٱلۡعُمُرِ لِكَيۡ لَا يَعۡلَمَ بَعۡدَ عِلۡمٖ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٞ قَدِيرٞ ﴾
[النَّحل: 70]
﴿والله خلقكم ثم يتوفاكم ومنكم من يرد إلى أرذل العمر لكي لا﴾ [النَّحل: 70]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Amewaumba, kisha Atawafisha katika mwisho wa umri wenu. Na kati yenu kuna wale ambao watafikia umri muovu, nao ni ukongwe, kama alivyokuwa uchangani mwake, hajui chochote ambacho alikuwa akikijua. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, ni muweza, ujuzi Wake na uweza wake vimezunguka kila kitu. Mwenyezi Mungu Aliyemrudisha mwanadamu kwenye hali hii ni muweza wa kumfisha kisha kumfufua |