×

Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa mtumwa aliye milikiwa, asiye weza kitu, na 16:75 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nahl ⮕ (16:75) ayat 75 in Swahili

16:75 Surah An-Nahl ayat 75 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 75 - النَّحل - Page - Juz 14

﴿۞ ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا عَبۡدٗا مَّمۡلُوكٗا لَّا يَقۡدِرُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَمَن رَّزَقۡنَٰهُ مِنَّا رِزۡقًا حَسَنٗا فَهُوَ يُنفِقُ مِنۡهُ سِرّٗا وَجَهۡرًاۖ هَلۡ يَسۡتَوُۥنَۚ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[النَّحل: 75]

Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa mtumwa aliye milikiwa, asiye weza kitu, na mwingine tuliye mruzuku riziki njema inayo toka kwetu, naye akawa anatoa katika riziki hiyo kwa siri na dhaahiri. Je, hao watakuwa sawa? Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ضرب الله مثلا عبدا مملوكا لا يقدر على شيء ومن رزقناه منا, باللغة السواحيلية

﴿ضرب الله مثلا عبدا مملوكا لا يقدر على شيء ومن رزقناه منا﴾ [النَّحل: 75]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na Mwenyezi Mungu Amepiga mfano, Akafafanua kwa mfano huo ubatilifu wa itikadi ya washirikina. Mfano wenyewe ni wa mtu aliyemilikiwa asiyeweza kujipitishia jambo asiyemiliki chochote, na mtu mwingine aliye huru, mwenye mali ya halali ambayo Mwenyezi Mungu Amemruzuku, anayemiliki kupitisha atakalo katika mali hayo, akawa anapeana kwa siri na kwa dhahiri. Je, kuna yoyote mwenye akili atakayesema kwamba watu wawili hawa wako sawa? Hivyo ndivyo Alivyo Mwenyezi Mungu Anayemiliki na Anayepitisha. Yeye Hafanani na viumbe Vyake na watumwa wake. Basi vipi mtasawazisha baina yao? Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Yeye Ndiye Anayestahiki kushukuriwa na kusifiwa. Lakini wengi wa washirikina hawajui kwamba sifa njema na neema ni za Mwenyezi mungu na kwamba Yeye, Peke Yake, Ndiye Anayestahiki kuabudiwa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek