×

Na Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa watu wawili. Mmoja wao ni bubu, 16:76 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nahl ⮕ (16:76) ayat 76 in Swahili

16:76 Surah An-Nahl ayat 76 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 76 - النَّحل - Page - Juz 14

﴿وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا رَّجُلَيۡنِ أَحَدُهُمَآ أَبۡكَمُ لَا يَقۡدِرُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوۡلَىٰهُ أَيۡنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأۡتِ بِخَيۡرٍ هَلۡ يَسۡتَوِي هُوَ وَمَن يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ ﴾
[النَّحل: 76]

Na Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa watu wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo kwa bwana wake. Popote anapo muelekeza haleti kheri. Je! Huyo anaweza kuwa sawa na yule anaye amrisha uadilifu, naye yuko juu ya Njia Iliyo Nyooka

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وضرب الله مثلا رجلين أحدهما أبكم لا يقدر على شيء وهو كل, باللغة السواحيلية

﴿وضرب الله مثلا رجلين أحدهما أبكم لا يقدر على شيء وهو كل﴾ [النَّحل: 76]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na Mwenyezi Mungu Amepiga mfano mwingine wa ubatilifu wa ushirikina. Mfano wenyewe ni wa watu wawili, mmoja wao ni bubu kiziwi, haelewi wala haelezi, hawezi kujinufaisha yeye mwenyewe wala wengine, naye ni mzigo mzito kwa anyesimamia mambo yake na kumwangalia kwa mahitaji yake, akimtuma kwa jambo lolote alitekeleze hafaulu wala hamletei jambo lolote zuri. Na mtu mwengine ana hisia zilizo sawa, anajinufaisha yeye na wengine, anaamuru utunzaji wa haki, na yeye yuko kwenye njia iliyo wazi isiyopotoka. Je, watu wawili hawa wanalingana katika maoni ya wenye akili? Basi vipi mtasawazisha baina ya sanamu kiziwi na Mwenyezi Mungu Muweza Mwenye kuneemesha kila zuri
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek