Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 80 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۢ بُيُوتِكُمۡ سَكَنٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ بُيُوتٗا تَسۡتَخِفُّونَهَا يَوۡمَ ظَعۡنِكُمۡ وَيَوۡمَ إِقَامَتِكُمۡ وَمِنۡ أَصۡوَافِهَا وَأَوۡبَارِهَا وَأَشۡعَارِهَآ أَثَٰثٗا وَمَتَٰعًا إِلَىٰ حِينٖ ﴾
[النَّحل: 80]
﴿والله جعل لكم من بيوتكم سكنا وجعل لكم من جلود الأنعام بيوتا﴾ [النَّحل: 80]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na sifa za upungufu, Amewapatia nyinyi mapumziko na utulivu kwenye nyumba zenu pamoja na watu wenu mkiwa mijini, na Amewapatia nyinyi mahema na mindule ya ngozi za wanyama- howa, ambayo ni sahali kwenu mkiwa safarini, na ambayo ni sahali kwenu kuisimamisha pale mkaapo baada ya safari, na Amewapatia nyinyi kutokana na manyoya ya kondoo, manywele ya ngamia na nwyele za mbuzi vyombo vya matumizi yenu ya kuvaa, kujifinika, kutandika na pambo la nyinyi kujifurahisha kwalo mpaka kipindi kilichotajwa na wakati ujulikanao |