Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 84 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدٗا ثُمَّ لَا يُؤۡذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ ﴾
[النَّحل: 84]
﴿ويوم نبعث من كل أمة شهيدا ثم لا يؤذن للذين كفروا ولا﴾ [النَّحل: 84]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wakumbushe, ewe Mtume, yale yatakayokuwa Siku ya Kiyama, tutakapowaletea kila kundi la watu Mtume wao akitolea ushahidi Imani ya walioamini miongoni mwao na ukanushaji wa wenye kukanusha. Kisha hao waliokanusha hawatapewa nafasi ya kuomba msamaha kwa waliyoyafanya, na hawatatakiwa kumridhisha Mola wao kwa kutubia na kufanya matendo mema, kwani wakati wa hilo ushapita |