×

Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na 16:90 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nahl ⮕ (16:90) ayat 90 in Swahili

16:90 Surah An-Nahl ayat 90 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 90 - النَّحل - Page - Juz 14

﴿۞ إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَٱلۡإِحۡسَٰنِ وَإِيتَآيِٕ ذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَيَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِ وَٱلۡبَغۡيِۚ يَعِظُكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ ﴾
[النَّحل: 90]

Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن الله يأمر بالعدل والإحسان وإيتاء ذي القربى وينهى عن الفحشاء والمنكر, باللغة السواحيلية

﴿إن الله يأمر بالعدل والإحسان وإيتاء ذي القربى وينهى عن الفحشاء والمنكر﴾ [النَّحل: 90]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Anawaamrisha waja Wake ndani ya Qur’ani hii wawe waadilifu, wafanye usawa katika kutunza haki Yake, kwa kumpwekesha Yeye na kutomshirikisha, na haki ya waja Wake, kwa kumpa haki yake kila mwenye haki. Na Anaamrisha kufanya wema katika kutekeleza haki Yake, kwa kumuabudu na kutekeleza faradhi Zake kwa namna ilivyopasishwa na Sheria, na kuwafanyia wema viumbe Wake katika maneno na vitendo. Na Anaamrisha kuwapa walio na ukaribu wa ujamaa kitu cha kuwaunga na kuwatendea wema. Na Anakataza kila ambalo ni ovu, likiwa ni neno au ni tendo, na ambalo Sheria inalipinga na haikubaliani nalo la ukafiri na maasia, na kuwadhulumu watu na kuwafanyia maonevu. Na Mwenyezi Mungu, kwa maamrisho haya na makatazo haya, Anawaidhia na kuwakumbusha mwisho mbaya, ili mzikumbuke amri za Mweneyzi Mungu na mnufaike nazo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek