Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 91 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَأَوۡفُواْ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ إِذَا عَٰهَدتُّمۡ وَلَا تَنقُضُواْ ٱلۡأَيۡمَٰنَ بَعۡدَ تَوۡكِيدِهَا وَقَدۡ جَعَلۡتُمُ ٱللَّهَ عَلَيۡكُمۡ كَفِيلًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا تَفۡعَلُونَ ﴾
[النَّحل: 91]
﴿وأوفوا بعهد الله إذا عاهدتم ولا تنقضوا الأيمان بعد توكيدها وقد جعلتم﴾ [النَّحل: 91]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na jilazimisheni kutekeleza kila ahadi mliyojilazimisha nayo juu ya nafsi zenu, baina yenu nyinyi na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, au baina yenu na watu katika yale yasiyoenda kinyume na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Nabii Wake. Wala msirudi nyuma kwenye viapo mlivyovitilia mkazo, na hali mlimfanya Mwenyezi Mungu Ndiye mdhamini na msimamizi mlipomuahidi. Hakika Mwenyezi Mungu Anayajua mnayoyafanya na Atawalipa kwayo |