Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 60 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿وَإِذۡ قُلۡنَا لَكَ إِنَّ رَبَّكَ أَحَاطَ بِٱلنَّاسِۚ وَمَا جَعَلۡنَا ٱلرُّءۡيَا ٱلَّتِيٓ أَرَيۡنَٰكَ إِلَّا فِتۡنَةٗ لِّلنَّاسِ وَٱلشَّجَرَةَ ٱلۡمَلۡعُونَةَ فِي ٱلۡقُرۡءَانِۚ وَنُخَوِّفُهُمۡ فَمَا يَزِيدُهُمۡ إِلَّا طُغۡيَٰنٗا كَبِيرٗا ﴾
[الإسرَاء: 60]
﴿وإذ قلنا لك إن ربك أحاط بالناس وما جعلنا الرؤيا التي أريناك﴾ [الإسرَاء: 60]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kumbuka, ewe Mtume, pindi tulipokwambia kwamba Mola wako Amewazunguka watu kwa ujuzi na uweza. Na hatukuijaalia ndoto tuliyokuonyesha waziwazi usiku wa isrā’ (kwenda Bayt al- Maqdis) na mi'rāj (kupaa kwenda mbinguni) miongoni mwa maajabu ya viumbe isipokuwa ni kuwatahini watu. Na tunawatisha washirikina kwa aina mbalimbali za adhabu na miujiza, lakini kuwatisha huko hakuwaongezei isipokuwa ni kuendelea zaidi kwenye ukafiri na upotevu |