Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 7 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿إِنۡ أَحۡسَنتُمۡ أَحۡسَنتُمۡ لِأَنفُسِكُمۡۖ وَإِنۡ أَسَأۡتُمۡ فَلَهَاۚ فَإِذَا جَآءَ وَعۡدُ ٱلۡأٓخِرَةِ لِيَسُـُٔواْ وُجُوهَكُمۡ وَلِيَدۡخُلُواْ ٱلۡمَسۡجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٖ وَلِيُتَبِّرُواْ مَا عَلَوۡاْ تَتۡبِيرًا ﴾
[الإسرَاء: 7]
﴿إن أحسنتم أحسنتم لأنفسكم وإن أسأتم فلها فإذا جاء وعد الآخرة ليسوءوا﴾ [الإسرَاء: 7]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mkifanya matendo yenu na maneno yenu kuwa mazuri,basi mimejifanyia vizuri nyinyi wenyewe, kwa kuwa malipo ya hayo yatarudi kwenu; na mkifanya vibaya, basi mateso ya hayo ni yenye kuwarudia nyinyi. Na utakapofika wakati wa uharibifu wa pili, tutawasaliti maadui wenu mara nyingine, ili wawadhalilishe na wawashinde na idhihiri athari ya udhalilifu na utwevu kwenye nyuso zenu na wawaingilie kwenye Bayt al Maqdis waiharibu kama walivyoiharibu mara ya kwanza na wavunjevunje kila kilichoko chini ya mikono yao uvunjaji kamili |