Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 8 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يَرۡحَمَكُمۡۚ وَإِنۡ عُدتُّمۡ عُدۡنَاۚ وَجَعَلۡنَا جَهَنَّمَ لِلۡكَٰفِرِينَ حَصِيرًا ﴾
[الإسرَاء: 8]
﴿عسى ربكم أن يرحمكم وإن عدتم عدنا وجعلنا جهنم للكافرين حصيرا﴾ [الإسرَاء: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Inatarajiwa kuwa Mola wenu, enyi Wana wa Isrāīl, Atawarehemu baada ya kuwatesa, mkitubia na mkatengenea, na mkirudi kufanya uharibifu na maonevu, tutarudi kuwatesa na kuwadhili. Na tumeufanya moto wa Jahanamu, kwenu na kwa makafiri kwa jumla, ni gereza ambalo hakuna kutoka humo kabisa. Katika aya hii na ile kabla yake pana onyo kwa ummah huu dhidi ya kufanya maasia ili lisiwapate lile lililowapata Wana wa Isrāīl, basi mipango ya Mwenyezi Mungu ni mimoja, haina kubadilika wala kugeuka |