Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 93 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿أَوۡ يَكُونَ لَكَ بَيۡتٞ مِّن زُخۡرُفٍ أَوۡ تَرۡقَىٰ فِي ٱلسَّمَآءِ وَلَن نُّؤۡمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيۡنَا كِتَٰبٗا نَّقۡرَؤُهُۥۗ قُلۡ سُبۡحَانَ رَبِّي هَلۡ كُنتُ إِلَّا بَشَرٗا رَّسُولٗا ﴾
[الإسرَاء: 93]
﴿أو يكون لك بيت من زخرف أو ترقى في السماء ولن نؤمن﴾ [الإسرَاء: 93]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upande daraja za kukupaisha mbinguni, na hatutaamini kupaa kwako mpaka urudi ukiwa na kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kilichofunguliwa tusome ndani yake kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kikweli.» Sema, ewe Mtume, kwa kushangaa juu ya ushindani wa makafiri hawa, «Kutakata na sifa za upungufu ni kwa Mola wangu! Kwani mimi ni nani, isipokuwa ni mja miongoni mwa waja Wake mwenye kufikisha ujumbe Wake? Basi vipi mimi nitaweza kuyafanya mnayoyataka?» |