Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 97 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿وَمَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلۡمُهۡتَدِۖ وَمَن يُضۡلِلۡ فَلَن تَجِدَ لَهُمۡ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِهِۦۖ وَنَحۡشُرُهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ عُمۡيٗا وَبُكۡمٗا وَصُمّٗاۖ مَّأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ كُلَّمَا خَبَتۡ زِدۡنَٰهُمۡ سَعِيرٗا ﴾
[الإسرَاء: 97]
﴿ومن يهد الله فهو المهتد ومن يضلل فلن تجد لهم أولياء من﴾ [الإسرَاء: 97]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Anamuongoza ndiye mwenye kuongoka kwenye haki, na yoyote yule ambaye Yeye Anampoteza, Akamdhili na Akamuachia yeye na nafsi yake basi huyo hakuna mwenye kumuongoza badala ya Mwenyezi Mungu. Hawa wapotevu Mwenyezi Mungu Atawafufua Siku ya Kiyama na Awakusanye kwa nyuso zao hali wakiwa hawaoni wala hawatamki wala hawasikii. Mwisho wao ni moto wa Jahanamu wenye kuwaka, kila kutuliapo kuwaka kwake na kuzimika mroromo wake, tunawazidishia moto wenye kuwaka na kuroroma |