×

Na kwa namna hii tuliwainua usingizini wapate kuulizana wao kwa wao. Alisema 18:19 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Kahf ⮕ (18:19) ayat 19 in Swahili

18:19 Surah Al-Kahf ayat 19 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 19 - الكَهف - Page - Juz 15

﴿وَكَذَٰلِكَ بَعَثۡنَٰهُمۡ لِيَتَسَآءَلُواْ بَيۡنَهُمۡۚ قَالَ قَآئِلٞ مِّنۡهُمۡ كَمۡ لَبِثۡتُمۡۖ قَالُواْ لَبِثۡنَا يَوۡمًا أَوۡ بَعۡضَ يَوۡمٖۚ قَالُواْ رَبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِمَا لَبِثۡتُمۡ فَٱبۡعَثُوٓاْ أَحَدَكُم بِوَرِقِكُمۡ هَٰذِهِۦٓ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ فَلۡيَنظُرۡ أَيُّهَآ أَزۡكَىٰ طَعَامٗا فَلۡيَأۡتِكُم بِرِزۡقٖ مِّنۡهُ وَلۡيَتَلَطَّفۡ وَلَا يُشۡعِرَنَّ بِكُمۡ أَحَدًا ﴾
[الكَهف: 19]

Na kwa namna hii tuliwainua usingizini wapate kuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku. Wakasema: Mola wenu Mlezi anajua zaidi muda mlio kaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha zenu ende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa akuleteeni cha kukila. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala asikutajeni kabisa kwa yeyote

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وكذلك بعثناهم ليتساءلوا بينهم قال قائل منهم كم لبثتم قالوا لبثنا يوما, باللغة السواحيلية

﴿وكذلك بعثناهم ليتساءلوا بينهم قال قائل منهم كم لبثتم قالوا لبثنا يوما﴾ [الكَهف: 19]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na kama tulivyowalaza na tukawahifadhi muda huu mrefu, tuliwaamsha kutoka kwenye usingizi wao kama vile walivyokuwa bila kubadilika, ili waulizane wao kwa wao, «Ni muda gani tulikaa tukiwa tumelala hapa?» Baadhi yao wakasema, «Tumekaa siku moja au sehemu ya siku.» Na wengine ambao mambo yaliwachanganyikia walisema, «utegemezeni ujuzi wa hilo kwa Mwenyezi Mungu, kwani Mola wenu ni Mjuzi zaidi wa kipindi mlichokikaa, basi mtumeni mmoja wenu na pesa zenu hizi za fedha aende mjini kwetu aangalie ni mtu gani hapo mjini mwenye chakula kizuri zaidi na cha halali, na awaletee chakula kutoka kwake, na ajifichefiche akiwa na muuzaji katika kununua kwake ili tusigundulike na mambo yetu yakafichuka, na msijulikane kabisa na mtu yoyote
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek