×

Watasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na wanasema: Walikuwa 18:22 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Kahf ⮕ (18:22) ayat 22 in Swahili

18:22 Surah Al-Kahf ayat 22 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 22 - الكَهف - Page - Juz 15

﴿سَيَقُولُونَ ثَلَٰثَةٞ رَّابِعُهُمۡ كَلۡبُهُمۡ وَيَقُولُونَ خَمۡسَةٞ سَادِسُهُمۡ كَلۡبُهُمۡ رَجۡمَۢا بِٱلۡغَيۡبِۖ وَيَقُولُونَ سَبۡعَةٞ وَثَامِنُهُمۡ كَلۡبُهُمۡۚ قُل رَّبِّيٓ أَعۡلَمُ بِعِدَّتِهِم مَّا يَعۡلَمُهُمۡ إِلَّا قَلِيلٞۗ فَلَا تُمَارِ فِيهِمۡ إِلَّا مِرَآءٗ ظَٰهِرٗا وَلَا تَسۡتَفۡتِ فِيهِم مِّنۡهُمۡ أَحَدٗا ﴾
[الكَهف: 22]

Watasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na wanasema: Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao. Wanavurumisha ovyo. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anaye jua sawa sawa hisabu yao. Hawawajui ila wachache tu. Basi usibishane juu yao ila kwa mabishano ya juu juu tu hivi. Wala usiulize khabari zao kwa yeyote yule

❮ Previous Next ❯

ترجمة: سيقولون ثلاثة رابعهم كلبهم ويقولون خمسة سادسهم كلبهم رجما بالغيب ويقولون سبعة, باللغة السواحيلية

﴿سيقولون ثلاثة رابعهم كلبهم ويقولون خمسة سادسهم كلبهم رجما بالغيب ويقولون سبعة﴾ [الكَهف: 22]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Watasema baadhi ya Watu wa Kitabu wenye kujishughulisha na mambo yao kwamba wao ni watatu na wa nne wao ni mbwa wao, na kundi lingine litasema kwamba wao ni watano na wa sita wao ni mbwa wao. Maneno ya makundi mawili haya ni maneno ya kudhania bila dalili yoyote. Na kundi la tatu litasema kwamba wao ni saba na wa nane wao ni mbwa wao. Sema, ewe Mtume, «Mola wangu Ndiye Mjuzi kabisa wa idadi yao,» hakuna anayeijua idadi yao isipokuwa ni wachache kati ya viumbe Wake. Basi usibishane na Watu wa Kitabu kuhusu idadi yao isipokuwa ubishi wa juu-juu usiokuwa na undani kwa kuwasimulia yale ambayo Mwenyezi Mungu amekuletea wahyi nayo, na usiulize kuhusu idadi yao na hali zao kwani wao hawalijui hilo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek