×

Na namna hivi tuliwa juulisha kwa watu wapate kujua ya kwamba ahadi 18:21 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Kahf ⮕ (18:21) ayat 21 in Swahili

18:21 Surah Al-Kahf ayat 21 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 21 - الكَهف - Page - Juz 15

﴿وَكَذَٰلِكَ أَعۡثَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ لِيَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَأَنَّ ٱلسَّاعَةَ لَا رَيۡبَ فِيهَآ إِذۡ يَتَنَٰزَعُونَ بَيۡنَهُمۡ أَمۡرَهُمۡۖ فَقَالُواْ ٱبۡنُواْ عَلَيۡهِم بُنۡيَٰنٗاۖ رَّبُّهُمۡ أَعۡلَمُ بِهِمۡۚ قَالَ ٱلَّذِينَ غَلَبُواْ عَلَىٰٓ أَمۡرِهِمۡ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيۡهِم مَّسۡجِدٗا ﴾
[الكَهف: 21]

Na namna hivi tuliwa juulisha kwa watu wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipo kuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao walisema: Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema. Wakasema walio shinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutawajengea msikiti juu yao

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وكذلك أعثرنا عليهم ليعلموا أن وعد الله حق وأن الساعة لا ريب, باللغة السواحيلية

﴿وكذلك أعثرنا عليهم ليعلموا أن وعد الله حق وأن الساعة لا ريب﴾ [الكَهف: 21]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na kama vile tulivyowalaza miaka mingi na tukawaamsha baada yake, tuliwafanya wajulikane na watu wa zama hizo baada ya muuzaji kuzigundua aina ya dirhamu alizozileta yule aliyetumwa na wao, ili watu wapate kujua kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ya Ufufuzi ni kweli na kwamba Kiyama hakina shaka ni chenye kuja. Kitahamaka hao waliowagundua watu wa Pango wakawa ni wenye kushindana kuhusu jambo la Kiyama: kuna waliolikubali na kuna waliolipinga. Na Mwenyezi Mungu Akajaalia kule kuwagundua watu wa Pango ni hoja kwa Waumini juu ya makafiri. Na baada ya mambo yao kugnuduliwa na wakafa, lilisema kundi moja la wale waliowagundua, «Jengeni kwenye mlango wa pango jengo la kuwasitiri kisha muwawache na mambo yao, Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa hali yao.» Na wakasema wale wenye kusikizwa maneno yao na wenye uwezo miongoni mwao, «Tutatengeneza mahali pao hapo msikiti wa kufanya ibada.» Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alikataza kuyafanya makaburi ya Manabii na watu wema kuwa misikiti, na alimlaani mwenye kufanya hivyo katika nyasia zake za mwisho kwa umati wake. Pia alikataza kabisa kujenga juu ya makaburi na kuyajengea na kuandika juu yake, kwani yote hayo ni miongoni mwa upitaji kiasi unaopelekea kuwaabudu waliomo ndani
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek