Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 27 - الكَهف - Page - Juz 15
﴿وَٱتۡلُ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَٰتِهِۦ وَلَن تَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلۡتَحَدٗا ﴾
[الكَهف: 27]
﴿واتل ما أوحي إليك من كتاب ربك لا مبدل لكلماته ولن تجد﴾ [الكَهف: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na usome Qur’ani, ewe Mtume, ambayo Mwenyezi Mungu Amekuletea wahyi nayo, kwani hiyo Qur’ani ni Kitabu ambacho hakuna mwenye kuyageuza maneno yake kwa kuwa ni ya kweli na ya uadilifu, na hutapata isipokuwa kwa Mola wako mahala pa wewe kuhamia wala pa kujilinda |