Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 114 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ أَن يُذۡكَرَ فِيهَا ٱسۡمُهُۥ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَآۚ أُوْلَٰٓئِكَ مَا كَانَ لَهُمۡ أَن يَدۡخُلُوهَآ إِلَّا خَآئِفِينَۚ لَهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا خِزۡيٞ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 114]
﴿ومن أظلم ممن منع مساجد الله أن يذكر فيها اسمه وسعى في﴾ [البَقَرَة: 114]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakuna dhalimu zaidi kuliko wale waliozuia kutajwa Mwenyezi Mungu katika msikiti, kama kusimamisha Swala na kusoma Qur’ani na mengine mfano wa hayo, na wakafanya bidii kuifanya magofu kwa kuivunja au kuifunga au kwa kuwazuia Waumini kuijia. Madhalimu hao haikuwa yapasa kwao kuingia hiyo msikiti isipokuwa wakiwa katika hali ya kuogopa na kutishika wasipate adhabu. Kwa matendo yao hayo, watakuwa na unyonge na fedheha ulimwenguni, na watakuwa na adhabu kali kesho Akhera |