Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 119 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗاۖ وَلَا تُسۡـَٔلُ عَنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡجَحِيمِ ﴾
[البَقَرَة: 119]
﴿إنا أرسلناك بالحق بشيرا ونذيرا ولا تسأل عن أصحاب الجحيم﴾ [البَقَرَة: 119]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sisi tumekutumiliza, ewe Mtume, kwa Dini ya haki iliyotiliwa nguvu kwa hoja na miujiza. Basi ifikishe kwa watu, pamoja na kuwapa Waumini bishara ya kheri ya dunia na ya Akhera, na kuwatisha wakaidi na adhabu ya Mwenyezi Mungu inayowangojea. Na baada ya kufikisha ujumbe, hutaulizwa juu ya ukafiri wa wenye kukukanusha. Wao wataingia Motoni, Siku ya Kiyama, wala hawatatoka humo |