×

Na walisema wale wasio jua kitu: Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au 2:118 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:118) ayat 118 in Swahili

2:118 Surah Al-Baqarah ayat 118 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 118 - البَقَرَة - Page - Juz 1

﴿وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ لَوۡلَا يُكَلِّمُنَا ٱللَّهُ أَوۡ تَأۡتِينَآ ءَايَةٞۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّثۡلَ قَوۡلِهِمۡۘ تَشَٰبَهَتۡ قُلُوبُهُمۡۗ قَدۡ بَيَّنَّا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يُوقِنُونَ ﴾
[البَقَرَة: 118]

Na walisema wale wasio jua kitu: Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au zikatufikia Ishara. Kama hivyo walisema wale walio kuwa kabla yao mfano wa kauli yao hii. Nyoyo zao zimefanana. Hakika Sisi tumeziweka wazi Ishara kwa watu wenye yakini

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وقال الذين لا يعلمون لولا يكلمنا الله أو تأتينا آية كذلك قال, باللغة السواحيلية

﴿وقال الذين لا يعلمون لولا يكلمنا الله أو تأتينا آية كذلك قال﴾ [البَقَرَة: 118]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Walisema wajinga miongoni mwa Watu wa Kitabu na wengineo kumwambia Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad, rehema na amani zimshukie, kwa njia ya inadi, “Si aseme na sisi Mwenyezi Mungu moja kwa moja Atuambie kwamba wewe ni Mtume Wake au itujie miujiza itokayo kwa Mwenyezi Mungu yenye kuonyesha ukweli wako.” Neno kama hili walilisema ummah waliopata kuwaambia Mitume wao, kwa njia ya ukaidi na ujeuri, kwa sababu ya kufanana nyoyo za waliotangulia na waliofuata katika ukafiri na upotevu. Hakika Tumezifafanua aya kwa wale wanaoamini Imani ya kikweli, kwa kumuamini kwao Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kuzifuata kwao Sheria Alizowawekea
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek