×

Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu 2:140 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:140) ayat 140 in Swahili

2:140 Surah Al-Baqarah ayat 140 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 140 - البَقَرَة - Page - Juz 1

﴿أَمۡ تَقُولُونَ إِنَّ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطَ كَانُواْ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰۗ قُلۡ ءَأَنتُمۡ أَعۡلَمُ أَمِ ٱللَّهُۗ وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَٰدَةً عِندَهُۥ مِنَ ٱللَّهِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ ﴾
[البَقَرَة: 140]

Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zao walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliye ficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo

❮ Previous Next ❯

ترجمة: أم تقولون إن إبراهيم وإسماعيل وإسحاق ويعقوب والأسباط كانوا هودا أو نصارى, باللغة السواحيلية

﴿أم تقولون إن إبراهيم وإسماعيل وإسحاق ويعقوب والأسباط كانوا هودا أو نصارى﴾ [البَقَرَة: 140]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Au je, Mnasema, kwa njia ya kujadili kuhusu Mwenyezi Mungu kwamba Ibrāhīm na Ismā'īl na Is’ḥāq na Ya’qūb na Asbāṭ - Manabii waliokuwa katika makabila kumi na mbili ya Wana wa Isrāīl wanaotokana na wana wa Ya’qūb - walikuwa katika dini ya Kiyahudi au ya Kinaswara? Huu ni urongo. Kwani hao walitumilizwa na kufa kabla ya Taurati na Injili. Waambie, ewe Mtume, “Kwani ni nyinyi mnaoijua zaidi dini yao au ni Mwenyezi Mungu Aliyetukuka?” Na Mwenyezi Mungu Ameshaeleza katika Qur’ani kwamba wao walikuwa Waislamu wenye msimamo uliolingana sawa. Na hakuna yoyote dhalimu zaidi kuliko nyinyi mnapouficha ushahidi uliothibiti kwenu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kudai kinyume chake kwa kumzulia Mwenyezi Mungu urongo. Na Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika na chochote katika vitendo vyenu. Yeye ni Mwenye kuvidhibiti na ni Mwenye kuwalipa kwavyo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek