Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 139 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿قُلۡ أَتُحَآجُّونَنَا فِي ٱللَّهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمۡ وَلَنَآ أَعۡمَٰلُنَا وَلَكُمۡ أَعۡمَٰلُكُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُخۡلِصُونَ ﴾
[البَقَرَة: 139]
﴿قل أتحاجوننا في الله وهو ربنا وربكم ولنا أعمالنا ولكم أعمالكم ونحن﴾ [البَقَرَة: 139]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia Watu wa Kitabu, “Je mnajadiliana na sisi juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasa, hali ya kuwa Yeye ni Mola wa viumbe wote, hahusiki na watu fulani tu bila ya wengine? Sisi tuna amali zetu, na nyinyi muna zenu. Na sisi tunamtakasia Mwenyezi Mungu ibada na utiifu; hatumshirikishi kitu chochote na hatumuabudu yoyote isipokuwa Yeye.” |