Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 144 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿قَدۡ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجۡهِكَ فِي ٱلسَّمَآءِۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبۡلَةٗ تَرۡضَىٰهَاۚ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَحَيۡثُ مَا كُنتُمۡ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ شَطۡرَهُۥۗ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ لَيَعۡلَمُونَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا يَعۡمَلُونَ ﴾
[البَقَرَة: 144]
﴿قد نرى تقلب وجهك في السماء فلنولينك قبلة ترضاها فول وجهك شطر﴾ [البَقَرَة: 144]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika Tunauona mzunguko wa uso wako upande wa mbinguni mara baada ya mara, huku ukingojea kuteremka Wahyi juu yako kuhusiana na Kibla. Basi hakika Tutakuepusha na Baitul Maqdis Tukuelekeze kwenye kibla unachokipenda na unachokiridhia, nacho ni upande wa Msikiti wa Ḥarām ulioko Makkah. Basi, elekeza uso wako huko. Na popote mtakapokuwa, enyi Waislamu, na mkataka kuswali, elekeeni upande wa Msikiti wa Haram. Na hakika wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa elimu ya Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara wanajua kwamba kugeuzwa kwako kuelekezwa Alkaba ndio haki iliyothibiti katika vitabu vyao. Na wala Mwenyezi Mungu hakuwa ni Mwenye kughafilika juu ya yale wayafanyayo hawa wapinzani wenye shaka, na Atawalipa kwayo |