×

Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu 2:143 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:143) ayat 143 in Swahili

2:143 Surah Al-Baqarah ayat 143 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 143 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَٰكُمۡ أُمَّةٗ وَسَطٗا لِّتَكُونُواْ شُهَدَآءَ عَلَى ٱلنَّاسِ وَيَكُونَ ٱلرَّسُولُ عَلَيۡكُمۡ شَهِيدٗاۗ وَمَا جَعَلۡنَا ٱلۡقِبۡلَةَ ٱلَّتِي كُنتَ عَلَيۡهَآ إِلَّا لِنَعۡلَمَ مَن يَتَّبِعُ ٱلرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِۚ وَإِن كَانَتۡ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى ٱلَّذِينَ هَدَى ٱللَّهُۗ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَٰنَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِٱلنَّاسِ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 143]

Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu. Na hatukukifanya kibla ulicho kuwa nacho ila tupate kumjua yule anaye mfuata Mtume na yule anaye geuka akarejea nyuma. Na kwa yakini hilo lilikuwa jambo gumu isipo kuwa kwa wale alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuipoteza Imani yenu. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa watu na Mwenye kuwarehemu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وكذلك جعلناكم أمة وسطا لتكونوا شهداء على الناس ويكون الرسول عليكم شهيدا, باللغة السواحيلية

﴿وكذلك جعلناكم أمة وسطا لتكونوا شهداء على الناس ويكون الرسول عليكم شهيدا﴾ [البَقَرَة: 143]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na kama tulivyowaongoza, enyi Waislamu, kwenye njia sahihi katika Dini, tumewafanya kuwa ni ummah bora ulio muadilifu, ili mue mashahidi juu ya ummah waliopita, kesho Akhera, kwamba Mitume wao waliwafikishia jumbe za Mola wao, na ili Mtume, kesho Akhera, awe vilevile ni shahidi juu yenu, kwamba yeye aliwafikishia ujumbe wa Mola wake. Wala hatukukifanya, ewe Mtume, kile kibla cha Baitul Maqdis ulichokuwa ukikielekea, kisha tukakugeuza tukakuelekeza Alkaba (iliyopo Makkah) isipokuwa ni yapate kuonekana yale tuliyoyajua hapo kale, ujuzi unaofungamana na thawabu na adhabu, ili tumtenganishe yule ambaye atakufuata na kukutii na kuelekea pamoja nawe pale utakapoelekea na yule aliye dhaifu wa imani, awe ni mwenye kubadilika na kuritadi kwa kuacha Dini yake kwa shaka yake na unafiki wake. Hali hii ya kugeuka Muislamu katika Swala yake, kuacha kuelekea Baitul Maqdis na kuelekea Alkaba ni ngumu na nzito, isipokuwa kwa wale walioongozwa na Mwenyezi Mungu na kupewa neema ya Imani na uchajimungu. Na wala hakuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupoteza imani yenu Kwake na kumfuata kwenu Mtume Wake kwa kuzibatilisha Swala zenu mlipokuwa mnaelekea kibla cha zamani. Hakika Yeye Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na upungufu wowote na Aliyetukuka, kwa watu ni Mpole na Mwenye huruma
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek