Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 145 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَلَئِنۡ أَتَيۡتَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ بِكُلِّ ءَايَةٖ مَّا تَبِعُواْ قِبۡلَتَكَۚ وَمَآ أَنتَ بِتَابِعٖ قِبۡلَتَهُمۡۚ وَمَا بَعۡضُهُم بِتَابِعٖ قِبۡلَةَ بَعۡضٖۚ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ إِنَّكَ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[البَقَرَة: 145]
﴿ولئن أتيت الذين أوتوا الكتاب بكل آية ما تبعوا قبلتك وما أنت﴾ [البَقَرَة: 145]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau utawaletea wale waliopewa Taurati na Injili aina yoyote ya hoja na dalili kwamba kuelekea kwako Alkaba katika swala ndio haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hawangalikifuata kibla chako, kwa inadi na kiburi. Na wala wewe si mwenye kukifuata kibla chao mara nyingine. Wala baadhi yao si wenye kufuata kibla cha baadhi yao. Na lau utafuata matamanio ya nafsi zao kuhusu kibla na mengineyo, baada ya ujuzi uliyoupata kuwa wewe uko kwenye haki na wao wako kwenye batili, wewe wakati huo utakuwa ni miongoni mwa waliozidhulumu nafsi zao. Haya ni maelezo kuambiwa ummah wote, na ni kitisho na kemeo kwa kila afuataye matamanio ya wanaoenda kinyume na Sheria ya Kiislamu |