Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 156 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿ٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَٰبَتۡهُم مُّصِيبَةٞ قَالُوٓاْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّآ إِلَيۡهِ رَٰجِعُونَ ﴾
[البَقَرَة: 156]
﴿الذين إذا أصابتهم مصيبة قالوا إنا لله وإنا إليه راجعون﴾ [البَقَرَة: 156]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Miongoni mwa sifa za hawa wenye kusubiri ni kwamba wao wanapofikwa na kitu wanachokichukia husema, «Sisi ni waja waliomilikiwa na Mwenyezi Mungu, tunaoendeshwa kwa amri Yake na mapitisho Yake. Anafanya kwetu Alitakalo. Na sisi Kwake, Peke Yake, ni wenye kurudi kwa kufa, kisha kwa kufufuliwa ili kuhesabiwa na kulipwa |