Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 18 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿صُمُّۢ بُكۡمٌ عُمۡيٞ فَهُمۡ لَا يَرۡجِعُونَ ﴾
[البَقَرَة: 18]
﴿صم بكم عمي فهم لا يرجعون﴾ [البَقَرَة: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wao ni viziwi, hawaisikii haki kwa kuizingatia, ni mabubu, hawaitamki haki, ni vipofu, hawauoni mwangaza wa uongofu. Kwa hivyo, hawawezi kurudi kwenye Imani ambayo waliiacha na kuchukuwa upotevu badali yake |