Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 17 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿مَثَلُهُمۡ كَمَثَلِ ٱلَّذِي ٱسۡتَوۡقَدَ نَارٗا فَلَمَّآ أَضَآءَتۡ مَا حَوۡلَهُۥ ذَهَبَ ٱللَّهُ بِنُورِهِمۡ وَتَرَكَهُمۡ فِي ظُلُمَٰتٖ لَّا يُبۡصِرُونَ ﴾
[البَقَرَة: 17]
﴿مثلهم كمثل الذي استوقد نارا فلما أضاءت ما حوله ذهب الله بنورهم﴾ [البَقَرَة: 17]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hali ya wanafiki ambao wameuamini, kidhahiri sio kindani, utume wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye, kisha wakakanusha, wakawa wanaenda huku na kule kwenye giza la upotevu wao bila kujua wanapoenda wala kuwa na matarajio ya kutoka kwenye giza hilo, inafanana na hali ya kikundi cha watu, kwenye usiku wa giza, ambapo mmoja wao aliwasha moto mkubwa ili wapate joto na mwangaza. Moto ulipowaka na kung’arisha pambizo zake, ulizimika na giza likaenea. Wakawa watu hao wako kwenye giza, hawaoni chochote wala hawaongoki kupajua penye njia ya kujua matoko |