×

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, 2:185 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:185) ayat 185 in Swahili

2:185 Surah Al-Baqarah ayat 185 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 185 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿شَهۡرُ رَمَضَانَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ فِيهِ ٱلۡقُرۡءَانُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَٰتٖ مِّنَ ٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡفُرۡقَانِۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ ٱلشَّهۡرَ فَلۡيَصُمۡهُۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٖ فَعِدَّةٞ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَۗ يُرِيدُ ٱللَّهُ بِكُمُ ٱلۡيُسۡرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ ٱلۡعُسۡرَ وَلِتُكۡمِلُواْ ٱلۡعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ ﴾
[البَقَرَة: 185]

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru

❮ Previous Next ❯

ترجمة: شهر رمضان الذي أنـزل فيه القرآن هدى للناس وبينات من الهدى والفرقان, باللغة السواحيلية

﴿شهر رمضان الذي أنـزل فيه القرآن هدى للناس وبينات من الهدى والفرقان﴾ [البَقَرَة: 185]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwezi wa Ramadhani ambao Ameanza Mwenyezi Mungu kuteremsha Qur’ani katika usiku wa cheo na utukufu, laylatul qadr, ilii kuwaongoza watu kwenye haki. Ndani yake Amezifungua wazi dalili za uongofu wa Mwenyezi Mungu na upambanuzi baina ya haki na batili. Kwa hivyo, mtu atakayeufikia mwezi huo, akawa ni mzima na mkazi wa mjini, basi na aufunge mchana wake. Mgojwa na msafiri wanaruhusiwa kufungua, kisha walipe idadi ya siku walizofungua. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anawatakia usahali na wepesi katika Sheria Zake, wala Hawatakii uzito na mashaka, na ili mupate kukamilisha idadi ya kufunga mwezi mzima na mumalize kufunga kwa kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu katika Idi ya Mfungo na mpate kumshukuru juu ya zile neema Alizowaneemesha nazo za uongofu, taufiki na usahali
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek