×

(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au 2:184 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:184) ayat 184 in Swahili

2:184 Surah Al-Baqarah ayat 184 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 184 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿أَيَّامٗا مَّعۡدُودَٰتٖۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٖ فَعِدَّةٞ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَۚ وَعَلَى ٱلَّذِينَ يُطِيقُونَهُۥ فِدۡيَةٞ طَعَامُ مِسۡكِينٖۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيۡرٗا فَهُوَ خَيۡرٞ لَّهُۥۚ وَأَن تَصُومُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ﴾
[البَقَرَة: 184]

(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua

❮ Previous Next ❯

ترجمة: أياما معدودات فمن كان منكم مريضا أو على سفر فعدة من أيام, باللغة السواحيلية

﴿أياما معدودات فمن كان منكم مريضا أو على سفر فعدة من أيام﴾ [البَقَرَة: 184]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Amewafaradhia Mwenyezi Mungu kufunga siku zinazojulikana idadi yake, nazo ni siku za mwezi wa Ramadhani. Basi yule kati yenu atakuwa mgonjwa, ikawa ni uzito kwake kufunga, au akawa ni msafiri, basi aweza kufungua. Na itamlazimu kufunga idadi ya siku nyengine zinazolingana na idadi ya siku alizokula. Na ni juu ya wale ambao kwao ni vigumu kufunga na ikawa inawaelemea maelemeo yasiyochukulika, kama mzee mkongwe na mngonjwa asiyetarajiwa kupoa, watoe fidiya ya kila siku ambayo watafungua, nayo ni kulisha masikini. Na yule atakayezidisha katika kiwango cha fidiya, kwa hiyari yake, basi hilo ni bora kwake. Na kufunga kwenu ni bora kwenu, pamoja na kuhimili shida, kuliko kutoa fidiya, iwapo mnazijua fadhila kubwa zipatikanazo kwenye kufunga mbele ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek