Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 189 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿۞ يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡأَهِلَّةِۖ قُلۡ هِيَ مَوَٰقِيتُ لِلنَّاسِ وَٱلۡحَجِّۗ وَلَيۡسَ ٱلۡبِرُّ بِأَن تَأۡتُواْ ٱلۡبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَٰكِنَّ ٱلۡبِرَّ مَنِ ٱتَّقَىٰۗ وَأۡتُواْ ٱلۡبُيُوتَ مِنۡ أَبۡوَٰبِهَاۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ ﴾
[البَقَرَة: 189]
﴿يسألونك عن الأهلة قل هي مواقيت للناس والحج وليس البر بأن تأتوا﴾ [البَقَرَة: 189]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wanakuuliza watu wako, ewe Nabii, kuhusu miezi michanga na kubadilika hali zake. Waambie, Mwenyezi Mungu Ameifanya miezi kuwa ni alama za watu kujua nyakati za ibada zao zilizowekewa wakati, mfano wa Saumu na Hija, na nyakati za kuamiliana kwao. Kheri haiko katika mambo mliyoyazowea wakati wa ujahilia na mwanzo wa Uislamu ya kuingia majumbani kupitia kwa nyuma, wakati mnapotia nia ya Hija au ya Umra, mkidhani kwamba huko ndiko kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Lakini kheri ni kile kitendo cha mwenye kumcha Mwenyezi Mungu na akajiepusha na maasia. Na ingieni majumbani kupitia kwenye milango yake wakati mnapohirimia Hija au Umra. Na muogopeni Mwenyezi Mungu katika mambo yenu yote ili mupate kufaulu kuyapata yote mnayoyapenda ya kheri ya dunia na ya Akhera |