×

Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni 2:194 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:194) ayat 194 in Swahili

2:194 Surah Al-Baqarah ayat 194 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 194 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿ٱلشَّهۡرُ ٱلۡحَرَامُ بِٱلشَّهۡرِ ٱلۡحَرَامِ وَٱلۡحُرُمَٰتُ قِصَاصٞۚ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ عَلَيۡكُمۡ فَٱعۡتَدُواْ عَلَيۡهِ بِمِثۡلِ مَا ٱعۡتَدَىٰ عَلَيۡكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ ﴾
[البَقَرَة: 194]

Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: الشهر الحرام بالشهر الحرام والحرمات قصاص فمن اعتدى عليكم فاعتدوا عليه بمثل, باللغة السواحيلية

﴿الشهر الحرام بالشهر الحرام والحرمات قصاص فمن اعتدى عليكم فاعتدوا عليه بمثل﴾ [البَقَرَة: 194]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kuwapiga kwenu vita, enyi Waumini, hao washirikina, katika mwezi ambao Mwenyezi Mungu Ameharamisha vita, ni malipo ya wao kuwapiga nyinyi vita mwezi mtukufu.Na yule anayekeuka yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu ya pahali na zama, atapewa mateso yanayofanana na kitendo chake na yanayotokana na jinsi ya kosa alilolifanya. Basi atakayewafanyia uadui kwa vita au chinginecho, wapeni adhabu ifananayo na uovu wao, wala pasiwe na dhiki kwenu kuhusu hilo. kwa sababu wao ndio wenye kuanza uadui. Na muogopeni Mwenyezi Mungu na msipitishe kipimo cha kufanana kuadhibu. Na juenu kuwa Mwenyezi Mungu Yuko pamoja na wale wamchao na wanaomtii kwa kutekeleza Aliyoyafanya faradhi na kuyaepuka Aliyoyafanya haramu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek