Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 195 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَأَنفِقُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا تُلۡقُواْ بِأَيۡدِيكُمۡ إِلَى ٱلتَّهۡلُكَةِ وَأَحۡسِنُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ﴾
[البَقَرَة: 195]
﴿وأنفقوا في سبيل الله ولا تلقوا بأيديكم إلى التهلكة وأحسنوا إن الله﴾ [البَقَرَة: 195]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na endeleeni, enyi Waumini, kutoa mali kwa kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kupigana jihadi katika njia yake. Wala msiziingize nafsi zenu kwenye maangamivu kwa kuacha jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuacha kutoa katika njia Yake. Na fanyeni wema katika kutoa na kutii, na mzifanye amali zenu zote ni zenye kutakasika kwa kukusudiwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Kwa hakika Mwenyezi Mungu Anawapenda watu wenye kutakasa nia na kufanya wema |